Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Sayyid Ammar Hakim, kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Taifa ya Iraq, ambaye alisafiri Tehran kwa ajili ya mazungumzo na wakuu wa Iran, alikutana na Ayatullah Sadiq Amoli Larijani, Rais wa Baraza la Uhakiki wa Maslahi ya Taifa la Iran.
Ayatullah Amoli Larijani katika mkutano huo, baada ya kutoa shukrani kwa ushirikiano wa ndugu zao wa Iraq, alibainisha kwamba; muungano wa mataifa haya miwili hauwezi kuharibika. Aidha, alibainisha umuhimu wa kuendelea kuwa makini dhidi ya njama za kutengeneza mgawanyiko wa maadui, ambazo zinafanywa kwa lengo la kudhoofisha mamlaka ya nchi za Kiislamu, ikiwemo Iraq. Alisema: Lengo la Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuishinikiza Hashd al-Shaabi ni kuandaa ardhi kwa ajili ya kugawanya au kudhoofisha nchi za eneo hili ili kuunda Israel Kuu.
Rais wa Baraza la Uhakiki wa Maslahi ya Taifa alibainisha baadhi ya sifa za Vita vya Siku 12, akasema: Katika vita hivi, ukweli mwingi umefahamika kwa wote. Adui aliingia uwanjani kwa uso wazi bila barakoa, na Wamarekani waliokuwa wakijitahidi kutetea mazungumzo, walionyesha asili yao halisi.
Akiashiria shambulio la adui dhidi ya nchi ya Irani wakati wa mazungumzo, alisisitiza: Vita hii imefanya baadhi ya watu ndani ya Iran, waliokuwa wakionyesha mfumo wa kisiasa kama kinyume na mazungumzo, kufikiria upya.
Ayatullah Amoli Larijani, akibainisha nguvu ya vikosi vya silaha na mshikamano wa wananchi wa Iran katika Vita vya Siku 12, alisema: Nguvu hii na mshikamano, imevunja ndoto na njama za wale ambao katika vikao vyao walikuwa wakipanga mfumo wa kisiasa baada ya Jamhuri ya Kiislamu.
Akiashiria hatua za busara za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika kuteua warithi wa maafisa mashahidi wa vikosi vya silaha, alisema: Katika vita hivi, mtazamo wa busara na shujaa wa Kamanda Mkuu wa Vikosi, pamoja na utendaji wa kishujaa wa vikosi vya silaha, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuonyesha uwezo wa makombora ya Iran, mshikamano wa kitaifa na msaada kamili wa wananchi kwa mfumo wa Kiislamu, ulizaa matokeo thabiti dhidi ya maadui.
Katika mkutano huo, Sayyid Ammar Hakim, kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Taifa ya Iraq, akibainisha fahari ya wananchi wa Iraq na mataifa ya Kiislamu kutokana na ushindi wa Iran katika Vita vya Siku 12, alisema: Kusimama kwa taifa la Iran dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni kumeimarisha nafasi ya Kimataifa ya Jamhuri ya Kiislamu na kuipa faraja dunia ya Kiislamu.
Aidha, alibainisha ukaribu wa ndugu wa mataifa ya Iran na Iraq, akasisitiza kuendeleza ushirikiano wa kila upande, hasa katika masuala ya biashara, na kumuombea Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, viongozi na wananchi wa Iran mafanikio mema.
Maoni yako